Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Nandy amesema wimbo wake mpya ‘Kivuruge’ ameununua.

Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na ngoma ‘Wasikundanye’ ameiambia Dj Show ya Radio One kutokana ngoma hiyo alinunua hivyo wale wanaosema wimbo huo amemuimbia mtu fulani wanakosea.
“Kivuruge hapana!!, sijamuimbia mtu kabisa, siyo true story ni wimbo ambao nimekuta umeshatungwa, mwenye wimbo anaitwa J Melody ambaye yupo pale THT alikuwa amesharekodi kila kitu then nilivyoisikia nikaipenda nikamwambia aniuzie, then akaniuzia ikiwa kama ilivyo” amesema Nandy.
Kivuruge ni ngoma ya pili kwa Nandy kutoa kwa mwezi huu mara baada ya kutoa ngoma ‘Mahabuba’ aliyomshirikisha Aslay.
 

Post a Comment

 
Top