Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Lucy Komba.
MKONGWE wa filamu nchini anayeishi Denmark, Lucy Komba amemtetea msanii mwenzake Irene Uwoya aliyefiwa na aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ na kuwataka watu kumuacha alie.

Irene Uwoya
Akizungumza na Za Motomoto News, Lucy alisema watu wanaomponda Uwoya kuhusiana na kifo cha Ndikumana wanakosea kwani hakuna mtu ambaye amewahi kufiwa na mume au aliyekuwa mzazi mwenzake na asilie.

“Kiukweli Uwoya mwacheni alie tu hata kama walikuwa wametengana, lakini unaposikia mtu ambaye aliwahi kuwa mume, mpenzi au baba watoto wako amefariki lazima uumie, tena sana kwani kifo ni kitu kingine kabisa, wanaomshambulia wamwache maana wanamuonea tu,” alisema Lucy.

Post a Comment

 
Top