Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
 Baraza la Sanaa Taifa(BASATA)limempongeza msanii wa muziki AT kwa ushindi wa tuzo za Mama Awards zilizofanyika nchini Marekani wiki iliyopita.
 AT alishinda tuzo mbili ambazo ni ‘International Artist’ na ‘Best Music Video’.
Kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Intagram wa baraza hilo imetoa pongezi kwa AT utokana na ushindi ailioupata na ubunifu.
 Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya mduara nchini Ally Ramadhani maarufu kwa jina la kisanii “AT” ameshinda Tuzo mbili za MAMAWARDS huko nchini Marekani.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama mlezi wa wasanii nchini linampongeza kwa dhati msanii “AT” pamoja na uongozi wake kwa heshima na sifa kubwa waliolipatia Taifa letu huko ughaibuni.
Aidha, BARAZA linapenda kuchukua nafasi hii kuwasihi wasanii nchini kuongeza ubunifu na ubora zaidi kwenye kazi zao ili sanaa yetu izidi kufika mbali zaidi kimataifa. #mamawards

Post a Comment

 
Top