Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MWANA-DADA anayefanya vizuri katika Bongo Fleva Faustina Charles ‘Nandy’ ameeleza kuwa hampendi mwanaume kwa sababu ya mkwanja isipokuwa anataka mapenzi ya kweli.


Akipiga stori na Risasi Vibes, Nandy ambaye anatamba na ngoma ya Kivuruge alisema anachopenda yeye ni mwanaume mcha Mungu na mchapakazi, haijalishi kama hiyo kazi inamuingizia kipato kikubwa au la.

“Fedha siyo kigezo cha mwanaume kuwa na mimi, muhimu mtu awe na hofu ya Mungu, asiwe mtu wa kujibweteka awe anajish-ughulisha kwa kazi yoyote ile, tutapambana wote kutafuta maisha hadi mambo yatakapokuwa vizuri na kujivunia kwa pamoja,”alisema.

Post a Comment

 
Top