Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanadada Faustina Charles ‘Nady’.
KWENYE sayari ya Bongo Fleva kwa sasa unapozungumzia wasanii wanaofanya poa huwezi kuacha kumtaja mwanadada Faustina Charles ‘Nady’ ambaye siku chache zilizopita alijinyakulia tuzo ya Afrima Kipengele cha Msanii Bora wa Kike, Afrika Mashariki nchini Sauz. Amani limezungumza naye baada ya kutwaa tuzo hiyo:

Amani: Mambo Nandy, una elimu gani na je, una mikakati yoyote ya kujiendeleza kimasomo?
Mwanadada Faustina Charles ‘Nady’ akiwa na tuzo yake.
Nandy: Nashukuru Mungu elimu niliyonayo si haba, nina Diploma ya Market nilisoma CBE lakini sijaishia hapo kuna mambo nayaweka sawa nikachukue Degree.

SHOWBIZ XTRA: Mbona umekomaa kwenye gemu la muziki pekee na siyo kufanya kazi ya ulichosomea?

Nandy: Sijawaza kufanya hivyo bado sababu sipendi kuajiriwa nimeshajiajiri mwenyewe, nina kampuni yangu ya mavazi asilia inaitwa Nandy African Queen, nashukuru Mungu inanisaidia kuendesha maisha yangu.

SHOWBIZ XTRA: Naona umetoa ngoma mpya Kivuruge ambayo ulisema umeitoa kama zawadi kwa mashabiki baada ya kukuomba utoe wakati ulikuwa hau hivyo, unaonaje mapokezi yake?
Nandy: Kivuruge imepokelewa vizuri kwa ukubwa niliotarajia sina budi kumshukuru Mungu kwa hilo, nadhani hiyo nd’o ngoma yangu ya kufungia mwaka sijajua bado kama nitatoa nyingine.

SHOWBIZ XTRA: Wasanii wengi wamekuwa wakianika wapenzi wao, kwa nini wewe hupendi kufanya hivyo kwa mashabiki wako wakamjua mtu wako?

Nandy: (Kicheko) ni kweli sijawahi kufikiria kumuanika mwanaume wangu, sababu sitaki kuchanganya maisha yangu ya muziki na maisha ya mapenzi naweza kuharibu kazi.

SHOWBIZ XTRA: Unajisikiaje kunyakua tuzo, ikiwa kuna baadhi ya wasanii wakongwe hawajawahi kufikia hatua hiyo?

Nandy: Najisikia furaha muda wote nilipoipata hadi sasa, naamini juhudi zangu ndio zimenifikisha kwenye hatua hiyo najivunia mno, hapa nilipo ni wakati wa kuongeza juhudi nipige hatua kubwa zaidi.

SHOWBIZ XTRA: Unawazungumziaje wakongwe kwenye gemu, kwani wapenda
burudani wengi kwa sasa macho yao yapo kwako na siyo kwa hao waliokut-angulia?

Nandy: Siwezi kuwasema vibaya, hakuna mkongwe niliomfunika kwanza. Nawaheshimu wote walionitangulia kila mtu na ladha yake kwa mashabiki, mimi nina ladha yangu na wao wana ladha yao kwa mashabiki wao, heshima yao inabaki palepale.

SHOWBIZ XTRA: Wasanii wengi wa kike kwa sasa wamelala, kutokana na tuzo uliyopata naamini umewapa kiu ya mafanikio, unawashauri nini ili waweze kurejea kwa kishindo?

Nandy: Sioni kama wamelala kila msanii ana malengo yake na namna ya kuuendesha muziki wake, hivyo siwezi jua mipangilio yao.

SHOWBIZ XTRA: Kutokana na levo uliyopo sasa, juhudi zako wengi wamekuwa wakikulinganisha na Vanessa Mdee, unamzungumziaje mwanadada huyo?

Nandy: Vanessa ni msichana mzuri anajituma mno, changamoto ni kawaida katika kazi.

SHOWBIZ XTRA: Wasanii wengi wamekuwa na wivu wa maendeleo, pale wanapoona msanii mwenzao anafanya vizuri je, unaonaje sapoti wanayokuonyesha wasanii wenzako inastahiki au wengi wanakuonea wivu?

Nandy: Sapoti ipo ya kutosha sijagundua utofauti wowote kwa wasanii wenzangu.

SHOWBIZ XTRA: Wazazi wako na familia yako kiujumla, wanakuchukuliaje baada ya kupata tuzo?
Nandy: Wazazi wangu wapo beneti na mimi tangu naanza muziki, hivyo baada ya kupata tuzo wamefurahi mno na wamezidi kunisapoti.

SHOWBIZ XTRA: Una chochote cha kuwaambia mashabiki wako?

Nandy: Nawapenda sana, bila wao nisingefika hapa nilipo, wazidi kunisapoti na wazidi kuniombea nipige hatua zaidi ya hapa nilipofika.

SHOWBIZ XTRA: Ahsante Nandy, Mungu abariki kipaji chako upate mafanikio zaidi ya hapo ulipofika.

Nandy: Nashukuru sana, karibu tena

Post a Comment

 
Top