Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwimbaji mpya wa Bongofleva Lulu Diva ambae mwaka huu umekua mwaka wake wa kwanza kupanda kwenye jukwaa la Tamasha la FIESTA, ameiambia Amplifaya ya CloudsFM kwamba amepewa taarifa za kuondolewa kwenye orodha ya Dar es salaam.

Mwanzoni alikuwepo kwenye orodha ya watakao-perform Jumamosi November 25 lakini kutokana na tamko la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kutoruhusu muziki kupigwa maeneo ya wazi Dsm kuanzia saa sita usiku na kuendelea, Lulu amesema jina lake limekatwa katika orodha hiyo na kurudishwa kwake ni iwapo FIESTAitaongezwa muda.
Lulu alisema imefanyika hivyo sababu orodha iliyoandaliwa awali ilipangwa kama ilivyopangwa kwenye mikoa mingine mwaka huu ambako tamasha hilo lilifanyika mpaka alfajiri na ndio maana anaiomba Serikali isaidie ili FIESTA ifanyike mpaka asubuhi.
“Mwaka huu ndio mwaka niliotimiza ndoto yangu na kutumbuiza kwa mara ya kwanza kwenye FIESTA, ujira wangu ninaopata pale ninagawana na kila mtu alie nyuma yangu, Dereva, Makeup Artist, Dancers wangu na wengine ndio maana naiomba Serikali kutufikiria tena sisi Wasanii” – Lulu Diva

Post a Comment

 
Top