Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Gift Stanford ‘Gigy Money’.

MWANAMUZIKI na muuza sura kwenye video mbalimbali za wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameeleza kuwa unene aliokuwa nao awali ulikuwa ni wa utoto hivyo kukonda kwake kwa sasa ni utu uzima.

Akizungumza na Za Motomoto News, Gigy Money alisema watu wanamsema kwa kukondeana kwake lakini anachoweza kusema ni kwamba unene wa zamani ulitokana na mwili wa kitoto lakini hivi sasa amekua mtu mzima
Akifanya yake kwenye shoo yake Mbeya.
“Katika familia yetu hakuna mtu mnene hata mmoja, wote ni wembamba hivyo ule mwili niliokuwa nao awali ulikuwa ni wa utoto lakini sasa hivi nimekua ndiyo maana nimepukutika na siyo vinginevyo kama watu wanavyonishambulia kwa maneno mabaya,” alisema Gigy Money.

Post a Comment

 
Top