Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili, kwa kosa la kumuua bila kukusudia Steven Kanumba, mastaa mbalimbali wameibuka na kumshauri asikate rufaa. Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa nyakati tofauti mastaa wa filamu pamoja na wanamuziki wameeleza sababu zao za kwa nini wanafikiri kuwa ni vyema Lulu akatumikia kifungo hicho.


Wengi wao wamesema kwamba miaka miwili sio mingi na kutokana na jinsi alivyokuwa akiishi bila kujua hatma yake, ni vyema akatumikia kifungo hicho ili akimaliza awe huru.

Msanii wa Bongo, Lulu Diva.
LULU DIVA: Nikipata nafasi ya kumshauri ama kuzungumza na Lulu ningemshauri bora atumikie tu kifungo chake ili awe huru, ana kila sababu ya kutumikia adhabu hiyo ili kupoza machungu ya mashabiki wa Kanumba na familia ya msanii huyo ambayo imekuwa na mtazamo tofauti kuhusu yeye.

SNURA Japo upo uwezekano wa kukata rufaa lakini mimi ninachoweza kumshauri kikubwa, anatakiwa kumwachia Mungu, aijuaye kesho yake ni Mungu peke yake
Msanii wa Bongo, Snura Mushi.
SANDRA: Asikate rufaa kwa sababu kesi inayohusiana na mauaji ni kesi kubwa, hata kama ataamua kukata rufaa kuna kuwa na mlolongo mrefu, hivyo uwezekano wa kutofanikiwa kwa rufaa yake ni mkubwa. Ni kheri atumikie kifungo ili baadaye awe mtu huru katika maisha yake mapya.

DAVINA: Asikate rufaa kwa sababu kuna watu ambao wanaona alifanya kosa, hivyo ni vema akatumikia hiyo miaka miwili kisha maisha yaendelee kama kawaida na Mungu atamsimamia. Asikate ili mambo yaishe atengeneze tu usawa!
Msanii wa Bongo Muvi, Davina.
MLELA: Mimi namshauri akabiliane na jaribu ili awe huru. Japokuwa jela sio pazuri lakini midomo ya watu na maneno mabaya yanatesa zaidi. Kila linalomtokea binadamu Mungu ndio hupanga kumpitisha katika jaribu hilo ili ampeleke mahali anapotaka awe.

PRETY CANDY: Ni vyema akatumikia tu kifungo maana kwa kweli mtazamo wa baadhi ya watu katika jambo hilo ni tofauti. Atumikie kifungo, akimaliza sidhani kama kuna mtu atakuwa na kinyongo naye tena.

MARY MAWIGI
Kwa upande wangu mimi namshauri tu amuombe Mungu atamfanyia wepesi maana ni miezi 18 tu atakaa Jela. Asikate tama, Mungu yu pamoja naye. Aidha, baadhi ya mastaa akiwemo Nuh Mziwanda, walionekana kumshauri tofauti Lulu kwa kumwambia akate tu rufaa kama anaona inafaa: “Binafsi naona ni haki yake ya msingi kukata rufaa, kwa kuwa sheria inampa haki hiyo namshauri akate rufaa kuliko kuendelea kuishi jela, ifahamike eneo lile siyo zuri kabisa. “Kama Lulu mwenyewe anaamini rufaa inaweza kumsadia juu ya msala huo ni bora akachukua hatua kuliko kuendelea kuteseka.”

Post a Comment

 
Top