Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mama Mzazi wa msanii wa filamu Bongo na Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Sepetu, ameenda Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye anapata matibabu nchini huyo.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amekuwa akitibiwa Nairobi tangu aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi Septemba mwaka huu.

Viongozi mbalimbali wa serikali na wa chama hicho wamekuwa wakienda kumjulia hali na sasa Mama wa Wema Sepetu amefanya hivyo.

Jana Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu, alimtembelea  Lissu hospitalini hapo. Mama Wema  na wanaye Februari 24 mwaka huu walitangaza kujiunga na Chadema.

Post a Comment

 
Top