Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Waziri Mwijage akizungumza na wanahabari.
ZAIDI ya Makampuni 500 yanatarajia kushiriki katika maonesho ya pili ya bidhaa za viwanda yanayotarajia kufanyika Desemba 7 hadi hadi 11, mwaka huu katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amesema katika maonyesho ya mwaka jana makampuni 472 pekee ndiyo yaliyoshiriki.
“Lengo kuu la maonesho haya ni kujenga jukwaa kwa wadau wa viwanda kupata fursa ya kujadiliana, kubadilisha uzoefu na kutangaza biashara za watanzania wote wanaomiliki viwanda vidogo, vya kati na vikubwa,” amesema Mwijage.

NA DENIS MTIMA/GPL

Post a Comment

 
Top