Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Judith Mbibo Wambura.
KAMA ilivyokuwa wakati walipotibuana, kwamba watu wachache walio karibu yao ndiyo waliojua chanzo, ndivyo inavyotokea tena sasa hivi inapofahamika kuwa bifu baina yao limeisha.Nawazungumzia ma-legend wawili katika Bongo Fleva, Judith Mbibo Wambura ambaye wengi tunamfahamu kama Lady Jaydee na Hamis Mwinjuma, hapa akifahamika zaidi kama Mwana FA.Na watu wasingejua kirahisi kama wawili hawa wako kwenye ugomvi kama siyo wote wawili kutangaza kufanya shoo kwa siku moja.
Jide alikuwa na onyesho lake la kutimiza miaka 13 katika Bongo Fleva ambayo ilipangwa kufanyika pale Nyumbani Lounge huku Mwana FA, akiitangaza siku hiyo kuwa na onyesho alilolipa jina la The Finest, ambalo lilipangwa kupigwa katika viwanja vya Makumbusho, kule Posta, jijini Dar. Hiyo ilikuwa ni Mei 2013.

Mwana FA.
Shoo zao hizo zilikuwa zipigwe Mei 31, 2013 lakini ghafla likaibuka tukio kubwa
Bongo Fleva, baada ya taarifa kuwa rapa mkali, bingwa wa freestyle Bongo, Albert Mangweha amefariki nchini Afrika Kusini.
Wote wawili wakatangaza kusitisha maonyesho yao kwa heshima ya mkali huyo, wakitaka umma wote uelekeze akili katika msiba huo wa kitaifa. Lakini kama sinema, wote kupitia akaunti zao za Twetter, wak-awaambia mashabiki wao kuwa watafanya onyesho lao June 15, 2013 katika viwanja vilevile vya awali!Masha-biki wa kweli wa muziki huu walipatwa na mshtuko mku-bwa kwa jambo hilo, kwani mion-goni mwa was-anii waliokuwa wakitoa ladha isiyoisha utamu masikioni, basi ilikuwa ni colabo ya nyimbo kati ya wawili hawa.
Na pengine, hii ndiyo sababu iliyofanya wafanye kazi nyingi pamoja (wanaweza kuwa ndiyo wasanii waliofanya kolabo nyingi kati yao kuliko wengine)Wamefanya kazi kadhaa ambazo zote zimewapa heshima kwa mashabiki kuanzia Wanaume Kama Mabinti, Alikufa Kwa Ngoma, Hawajui na Msiache Kuongea, achilia mbali Kibao cha Ama Zao Ama Zangu cha King Crazy GK, alichowashirikisha East Coast Team ya FA na Lady Jaydee. Na ukizisikiliza kazi zote hizi, japo ni za zamani, lakini haziwezi kuchuja ubora wake.
Kwa kuona jinsi wawili hawa walivyo pacha katika kazi zao, ndiyo maana rapa Albert Mangweha ‘Ngwear’ akawachukua ili kunogesha ngoma yake ya Sikiliza.
Isikilize Ngoma ya Hawajui kwa mfano, iliyofanywa karibu miaka tisa iliyopita, mali yake Mwana FA, uone jinsi wakongwe hawa walivyoonyesha kushibana kwao na hata ukiisikiliza leo, bado mashairi yake yanakuonyesha kuwa wao ni zaidi ya tunavyowafahamu!
FA anajaribu kumshawishi mkewe (Jide) aachane naye, kwani yeye (FA) ni kicheche, kila mwanamke anamtamani, ni malaya, hana sifa za kuwa naye kutokana na uvumilivu na mapenzi makubwa aliyonayo, lakini Jaydee, anatoa majibu yanayomshangazaHawajui tulipotoka, watajuaje tunapokwenda? Ya kwao yanawashinda yetu hawataweza..”Uzuri mmoja kwao ni kwamba chanzo cha bifu lao imebakia kuwa siri yao, kwani haikuwahi kuwekwa hadharani, kama tunavyosikia kuhusu ugomvi baina ya wasanii wengine. Pengine hii ilichangiwa zaidi na ‘uhenga’ wao, kwani hakuna aliyekuwa tayari kusema chanzo.
Kwa shabiki wa muda mrefu kidogo katika muziki huu, anajua ni kwa kiwango gani ‘kolabo’ ya wawili hawa ilivyopotea na kuufanya ukose ladha flani matata. Ni moja kati ya ‘chemistry’ chache ambazo hazijawahi kuchuja.
Kama kungekuwa na mashindano ya kukutanisha wasanii wanaoimba kwa kushirikiana na kutoa kitu ‘comfortable’ basi hii ingeibuka mshindi dhidi ya Sugu na Stara Thomas vibao (Sugu na Wanachotaka), Starehe na Nikusaidieje (Prof Jay ft Ferooz), Mikasi na Demu Wangu ( Ngweat ft Mchizi Mox) na Rostam (Roma Mkatoliki ft Stamina).
Kwamba bifu baina yao litabakia kuwa historia, ilianza mara tu baada ya Jide kutoa video ya kibao chake kipya, I Miss You na mara moja hasimu wake huyo akaiweka katika mtandao wake wa kijamii na kuwataka mashabiki kuupakua na kusikiliza, akiwawekea na link.
Kana kwamba haitoshi, siku chache baadaye, Jide akatupia picha katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii, ikimuonyesha akiwa pamoja na FA katika studio za B Hits, ambazo kwa miaka mingi, zimetumika kutoa kazi nyingi za rapa huyo.
Juu ya kupatana kwao, Malkia wa Afro Pop Afrika Mashariki, Lady Jaydee anasema; “Sisi ni watu wazima, tumefanya mambo mengi pamoja, hatuwezi kuwa na ugomvi wa kudumu kwa sababu hayakuwa mambo kihivyo, wakati umefika tumeamua kumaliza tofauti na maisha yanasonga mbele.”
Kuhusu kukutana kwao B Hits kama dalili za ujio wa ngoma mpya, anafunguka; “Yaaa, tuna mpango wa kufanya kazi tena, itakapokuwa tayari tutawafahamisha mashabiki.”
FA hakuweza kupatikana, lakini siku chache baada ya kumaliza bifu lao, alisikika katika kituo kimoja cha redio akisema wameondoa tofauti zao kwa sababu wao ni watu wazima na wameshafanya kazi nyingi pamoja.

STORI: RISASI VIBES | GLOBAL PUBLISHERS

Post a Comment

 
Top