Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mafundi umeme na Zimamoto wakiingia kupitia dirishani katika jengo la Clouds Media Group kuzima moto uliounguza baadhi ya ofisi leo jijini Dar es Salaam.
Juhudi za kuingia ndani zikiendelea.
Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (wa pili kulia, T-shirt ya bluu) akiwa na askari, wakiangalia juhudi za kuuzima moto uliotokea.
Akiongea na polisi.
Wafanyakazi wa Clouds na wananchi wakiwa nje ya jengo lililoshika moto.
Muonekano wa Jengo la Clouds Media Group.

Magari ya Zimamoto yaliyofika kupambana na moto huo.
SEHEMU  ya jengo la kituo cha Clouds Media Group lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam limeungua moto leo ambapo Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, amesema moto huo ulitokea bila ya mtu yeyote kuwa na taarifa nao ambapo ulianzia katika studio ndogo ya kurekodia.
Aliongeza kwamba kituo hicho si mara ya kwanza kupatwa majanga ya moto ambapo mara ya kwanza walipokuwa katika jengo la Kitegauchumi eneo la Posta jijini Dar es Salaam, moto uliteketeza studio zao na kupoteza vitu mbalimbali ambapo moto wa leo umeteketeza baadhi ya ofisi za studio ya Televisheni.
Hata hivyo, alikishukuru kikosi cha Zimamoto kwa kufika haraka eneo la tukio na kuuzima moto huo.  Vilevile alisema hakuna binadamu aliyepata madhara kutokana na tukio hilo.
Mutahaba alisema juhudi zaidi zinaendelea katika kituo hicho ili kurekebisha mambo yaliyotokea na kwamba ratiba zao zitaendelea kama kawaida.

Post a Comment

 
Top