Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes ameeleza sababu za kuupa jina la Bombardier wimbo wake mpya aliouachia wiki iliyopita.
Dully amesema ametumia jina la Bombardier kwa sababu ndege hizo zinasafiri umbali mrefu angani hivyo amejifananisha na yeye kwenye uwezo wake awapo faragha.

Bombardier ni ndege, tena ndege  kubwa ambazo zinakwenda juu umbali mrefu ambapo zinaweza kusimama kwa masaa 16 mpaka 18 juu angani. Kwa hiyo nimejifananisha mimi na Bombardier kwa sababu mimi ni mwanaume mwenye uwezo mkubwa kitandani nimejipa uanaume kwa  kutumia jina la Bombardier au kama wanavyosema mwanaume mashine.“amesema Dully Sykes kwenye mahojiano yake na Bongo5.
Wimbo mpya wa Bombardier wa Dully Sykes umepokelewa vizuri na wadau wa muziki kwani ni siku tatu tu tangu atoe video yake na tayari umetazamwa mara laki moja kwenye mtandao wa YouTube.
 

Post a Comment

 
Top