Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Ureno, Samuel Eto’o.
MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o, amekanusha ripoti kwamba alikodisha ndege ya kuwarudisha nchini Cameroon wananchi wenzake waliokuwa katika kile kilichoita utumwa nchini Libya.
Wanaodaiwa kuwa wakimbizi nchini Libya.
Picha zikionyesha ‘watumwa’ waliokondeana waliojazwa katika chumba kidogo na kisha baadaye kupanda ndege, zimekuwa zikionyeshwa katika mtandao wa Malachysblog, jambo ambalo mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Barceleona alikuwa kivutio kikubwa amelikanusha.
Hali ilivyo kwa ‘watumwa’ hao.
Baada ya kushuka kwenye ndege.
Posti iliyotumwa katika mtandao, inasema katika sehemu yake kwamba: “Samuel Eto’o alitumia mamilioni ya Dola alipokodisha ndege kwa wakimbizi wote wa Cameroon waliokuwa wamekwama Libya na walikuwa wanateswa na baadhi yao hadi kufa.”
Eto’o amekanusha ripoti hizi katika mtandao wa Facebook tarehe 24 Novemba na kusema hakusema atampa kila mkimbizi Dola milioni moja. Yote haya yanatokana na wimbi la Walibya kutaka kwenda Ulaya kwa ajii ya kutafufa maisha bora.

Post a Comment

 
Top