Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
PIX 1
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza jana Jijini Dar es Salaam katika sherehe za maadhimisho ya miaka 70 ya Uhuru wa Jamhuri ya India.

PIX 2.
Balozi wa India hapa nchini Mhe.San Deep Arya akizungumza jana Jijini Dar es Salaam  na wanachi waliojitokeza katika sherehe za  maadhimisho ya miaka 70 ya Uhuru waTaifa hilo.
PIX 3.PIX 4.PIX 5.
Burudani mbalimbali zikitumbuiza jana Jijini Dar es Salaam wakati wa shrehe za maadhimisho ya miaka 70 ya Uhuru wa Jamhuri ya India.
PIX 6
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akimpongeza mwalimu wa burudani wa ngoma za kihindi  jana Jijini Dar es Salaam katika sherehe za maadhimisho ya miaka 70 ya Uhuru wa nchi hiyo.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Jamhuri ya India kwa kutimiza miaka 70 tangu ilipopata Uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1947.
Waziri Mwakyembe ametoa pongezi hizo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za maadhimisho hayo ambapo ameipongeza nchi hiyo kwa kuendelea kuuenzi na kuulinda Utamaduni wao hata wakiwa nje ya India.
“Nawapongeza sana kwa kutimiza miaka 70 ya Uhuru ni jambo la kujivunia sana,lakini pia nawapongeza kwa kuendelea kuuenzi Utamaduni wenu kwa kila nyanja, na nawahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na nyie katika kuleta maendeleo miongoni mwetu.”Alisema Waziri Mwakyembe.
Naye Balozi wa India hapa nchini Mhe.SanDeep Arya emeishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika maeneo mbalimbali yenye manufaa kwa mataifa hayo mawili na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo wa kidiplomasia uliopo baina yao.
“India inafarijika sana na ushirikiano huu ulipo miongoni mwetu,tunaahidi kushirikiana zaidi hasa katika Sekta ya Utamaduni ambayo Serikali imeonyesha jitihada zake katika kuendeleza na kuimarisha kwa kuwa utamaduni ndio unaotambulisha mtu popote anapokuwa.”Alisema Balozi Arya.
Katika sherehe hizo watu waJamhuri ya India walionyesha Utamaduni wao kwa kucheza ngoma mbalimbali za Taifa hilo,nyimbo, pamoja na michezo mingine ya kihindi ikiwa ni kuendeleza na kudumisha Utamaduni wa nchi hiyo.

Post a Comment

 
Top