Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Producer kutoka studio za MJ Records, Daxo Chali amefunguka mambo kadhaa kuhusu ujio wa msanii Marlaw.

Daxo amesema kuwa ukimya wa Marlaw ulikuwa ni kutoa nafasi kwa yeye kusoma game kwa sababu huwezi kusoma game ukiwa ndani yake, hivyo wakati huo alikuwa anarekodi ngoma zake pole pole.
“Marlaw sasa hivi kawa mnyama zaidi, unakaa naye unatengeneza beat mpaka anakuwa kama anataka kushika hivi, yeah, anakuonyesha kuna vitu, so sikio lake kama limekua unajua ukiwa nje unakuwa unaona vitu vingi sana ni kama Alikiba alipoachia gape kuna kipindi, so ni kitu kama hicho hapo” Daxo ameiambia Funiko Base ya Radio5.
Daxo ameongeza kuwa katika ngoma tisa walizofanya hadi sasa hamna kolabo hata moja.

Post a Comment

 
Top