Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mwenyekiti wa CCM Taifa, John Pombe Magufuli.
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) ambayo inaendelea na vikao vyake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo iliwapokea na kuwarudisha katika chama hicho wanachama kadhaa kutoka vyama vya upinzani ambao walijitokeza mbele ya kujieleza na hatimaye kuomba kujiunga na chama hicho.Miongoni mwa wanachama walipokolewa ni Profesa Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, Edna Sunga (wote kutoka ACT-Wazalendo) (kutoka ACT-Wazalendo), Lawrence Masha na Patrobas Kitambi (Chadema) na wengineo.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, John Pombe Magufuli amewapongeza kwa kujiunga na kila alichosema chama bora na kinachowatetea wanyonge. Alisisitiza pia kwamba hatua yao ya kujiunga na chama hicho isije ikawa majaribio bali wahakikishe uamuzi wao huo uwe wa kudumu na wakitetee chama hicho kwa muda wote wa maisha yao.Wakati huohuo, baada ya Magufuli kuisomea NEC barua ya kuomba msamaha kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Sophia Simba, ambaye alifukuzwa uanachama mwaka huu, halmashauri hiyo ilimrudisha kwa kauli moja.

Post a Comment

 
Top