Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 

Meneja wa Nyanza Commercial Farm, Dilipkumar Pater ambae leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam imemuhukumu kwenda jela kwa miaka 20 baada ya kupatikana na hatia.

Pater amehukumiwa kwenda jela miaka 20 au kulipa faini ya Shilingi Milioni 534 baada ya kukutwa na kosa la kupatikana na kucha 17 za Simba.
Hukumu hiyo imetolewa leo November 22, 2017 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, ambapo amesema amesikiliza ushahidi uliotolewa na Mashahidi wanne wa upande wa mashtaka, vielelezo vitatu na utetezi wa Mshtakiwa mwenyewe.
Hakimu Mkeha amesema Mahakama imemkuta na hatia Mshtakiwa huyo baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi hiyo pasipo kuacha shaka na kueleza kuwa vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani hapo ni kucha za Simba, hati ya ukamataji na cheti cha kutathmini kucha hizo.
Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo mshtakiwa alishindwa kulipa faini na kupelekwa gerezani.

Post a Comment

 
Top