Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Bingwa wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua anaongoza katika orodha ya wachezaji 12 waliyotangazwa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2017 nchini Uingereza kupitia shirika la BBC.

Joshua mwenye umri wa miaka 28, ambae ni bingwa wazamani wa Olympic na bingwa wa uzito wa juu amekuwa akipendwa zaidi tangu alipotwaa taji lake la WBA na IBO baada ya kumshinda mpinzani wake Wladimir Klitschko katika dimba la Wembley mwezi Aprili.
Huku bondia huyo akifanikiwa kuutetea mkanda wake wa IBF katika pambano lake la hivi karibuni dhidi ya Carlos Takam mwezi Oktoba katika Uwanja wa Cardiff Principality uliyojaza mashabiki 80,000.
Anthony Joshua anakabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa bingwa wa mwaka  2014, Lewis Hamilton ambae pia ni mshindi mara nne wa mashindano ya Formula One mwezi uliyopita na Chris Froome mshindi mara nne wa mashindano ya Tour de France.
Dereva wa mashindano ya Formula One, Lewis Hamilton 
Mwanariadha, Mo Farah mshindi wa mbio za dunia mita 10,000 jijini London huku katika listi hiyo akiwemo mchezaji wa Tottenham, Harry Kane.
Kane ni mfungaji bora wa ligi ya Uingereza mwaka 2016/17 na kuisaidia Uingereza kufuzu michuano ya kombe la dunia.
Mchezaji tenis namba moja kwa ubora nchini Uingereza, Johanna Konta nimiongoni mwa wachezaji waliyotangazwa katika listi ya kuwania kinyang’anyiro hicho.
Chris Froome, who won his fourth Tour de France in the summer, is also a strong contender
Mwendesha baiskeli, Chris Froome mshindi mara nne wa Tour de France
Mo Farah, who won the world 10,000 metres title in London, is also on the 12-person short list
Mo Farah, bingwa wa dunia wa mbio za mita 10,000 jijini London
Harry Kane, the Premier League's top scorer in 2016-17 for the second season in a row, is listed
Harry Kane, mfungaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza mwaka 2016-17 
British women's tennis No 1 and Wimbledon semi-finalist Jo Konta is also among the nominees
Mchezaji tenis namba moja kwa viwango vya ubora nchini Uingereza, Jo Konta
Speed-skater Elise Christie is recognised for her successes at the World Championships
Mchezaji wa michezo ya katika barafu, Elise Christie
Jonathan Rea, who secured a third successive World Superbikes title, is also on the list
Jonathan Rea,
Jonnie Peacock makes the list after he secured gold at the IPC World Athletics Championships
Mwanariadha, Jonnie Peacock
Adam Peaty's achievements at the World Aquatics Championships have also been recognised
Muogeleaji, Adam Peaty
England women's cricketer Anya Shrubsole makes the list after they won the World Cup
Mchezaji kriketi mwanadada, Anya Shrubsole bingwa wadunia
Bianca Walkden (right), who defended her world taekwondo title, completes the 12-strong list
Bianca Walkden (kulia), bingwa wadunia wa mchezo wa taekwondo

Post a Comment

 
Top