Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ben Pol Afunguka Kolabo Yake na Wasanii Kadhaa Kutoka Ufaransa 
Msanii wa muziki wa R&B, Ben Pol amefunguka kwa kudai kwamba tayari amefanya kolabo na wasanii kadhaa kutoka nchini Ufaransa.


Muimbaji huyo alikuwa nchini humo wiki kadhaa zilizopita kwa mualiko maalum baada ya kuchaguliwa kuwa balozi na taasisi moja ya kusaidia watoto ya nchini humo.

Akiongeza na Bongo5 wiki hii, Muimbaji huyo ambaye anajipanga kuachia wimbo wa kufunga nao mwaka, amedai safari ya ufaransa aliitumia vizuri kwaajili ya muziki wake.

“Mungu ni mwema kuna kazi kadhaa nilibahatika kufanya lakini kwa sasa ni mapema zaidi kuzizungumzia,” alisema Ben Pol.

Aliongeza, “Muziki umekuwa na ushindani mkubwa hivyo ukipata nafasi lazima uitumie ipasavyo. Kwahiyo wakati nipo kule nilipata nafasi ya kukutana baadhi ya wadau na kufanikiwa kutengeneza baadhi ya kazi ambazo kwa sasa ni mapema zaidi kuzizungumzia,”

Muimbaji huyo alikuwa ni mmoja kati ya wasanii waliofanya vizuri weekend iliyopita katika tamasha kubwa la fiesta.

Post a Comment

 
Top