Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Tokeo la picha la baraka da prince na alikiba 
Kwa muda mrefu sasa wadau wengi wa muziki wa Bongo Fleva wamekuwa wakiamini kuwa Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince na mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba wana bifu au tofauti miongoni mwao baada ya Baraka The Prince kujitoa kwenye lebo ya RockStar4000 ambayo ipo chini ya Alikiba na Meneja wake Seven Mosha.

Ukweli ni kwamba Barakah The Prince hana tofauti/bifu  yoyote na Alikiba kama ambavyo mashabiki wengi wa Alikiba na wadau wa muziki walivyokuwa wakidhania kwani  Hitmaker huyo wa Sometimes kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha hilo kwa kumtakia Kheri ya siku yake ya kuzaliwa Alikiba .
Happy Birthday kaka King Kiba nakutakia maisha marefu“ameandika Barakah The Prince kwenye posti ambayo imeleta majibu kwa baadhi ya wadau waliokuwa wakidhani kuwa msanii huyo ana bifu na Alikiba.
Cheki maoni ya baadhi ya mashabiki wa Alikiba na wa muziki wa Bongo Fleva walivyotahamaki baada ya posti hiyo.
Alikiba leo Novemba 29, 2017 anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na mastaa kibao wamemposti kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kumtakia maisha kheri akiwemo Ommy Dimpoz, Mwana FA, na wengineo.

 

Post a Comment

 
Top