Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Zipu ya suruali ikiwa imefunguka.
DAR ES SALAAM: Hapo vepee! Ndivyo walivyosikika wapenda ubuyu, wakimuelekezea vidole, mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ aliyekuwa ameacha zipu yake wazi.

Kituko hicho cha aina yake kilichukua nafasi hivi karibuni maeneo ya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kulipokuwa na Tamasha la Fiesta.
Mpenda ubuyu mmoja aliyekuwa akimfuatilia kwa ukaribu, alimtonya paparazi wetu kuwa zipu ya Afande haipo sawa tangu akiwa jukwaani anakamua nyimbo zake kali zilizowakumbusha mbali mashabiki.
“Hebu mcheki ile zipu Afande Sele niaje? Ile ni staili au vipi? Hata kama ni staili ile yake imezidi aisee huwezi kuacha zipu wazi bhana maana lile ndilo eneo nyeti kwa kila mwanadamu,” alisikika mpenda ubuyu huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ally huku mwenzake aliyekuwa naye akimsapoti.
Paparazi wetu kwa umakini mkubwa alianza kumfuatilia Afande Sele na kumtandika picha akiwa angali jukwaani hadi aliposhuka nyuma ya jukwaa na kubaini kweli zipu hiyo ipo wazi alipokuwa amekaa karibu na mrembo mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja.
Hata hivyo, jitihada za mwanahabari wetu kuzungumza na Afande ziligonga mwamba kufuatia kuzongwa na watu muda huo kisha akatokomea kusikojulikana.
Hata baadaye alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi, iliita bila kupokelewa.

Post a Comment

 
Top