Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa Bongo Flava, Vanessa Mdee amedai kuwa haamini katika kujichubua ili kubadili rangi ya ngozi yake.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Kisela’ ameiambia Dj Show ya Radio One wengi wanaofanya hivyo ni wale waliokosa kujiamini.
“Mimi kama Vanessa siamini kwenye kujikoboa, kujichubua au kujibadilisha kwenye rangi yako ya kawaida au mwili wako wa kawida am belief in temporary, so ukaweka make-up au nywele kuongeza hiyo ni kitu temporary ambayo ukiamua usiku unatoa lakini vile vitu vya kufanya moja kwa moja siviamini,” amesema Vanessa.

“Na pia ile ishu ya confidence, mtu ukiwa in secured inaweza ukafanya hivyo vitu ukiwa unataka kujiboresha au kujiridhisha mwenyewe ukidhania ukijibadilisha utakuwa bora zaidi but I don’t think I need to do that,” ameongeza.

Vanessa ameendelea kwa kusema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na imani yake na dini imekataza na anachofanya yeye ni kumshukuru kwa hatua aliyofikia sasa.

Post a Comment

 
Top