Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

NADHANI KAMA KUNA KITU KINATIA FURAHA KWA SASA NIKUONE KIJANA AMBAYE ALIKUWA KAMA ANAONEKANA ANAPOTEA ANARUDI KWENYE RAMANI KWA KASI KUBWA.


Kijana ambaye ki muonekano ni kijana mstaarabu ambaye alikuwa anataka kuchafua muonekano wake na kuonekana kama muhuni katika wahuni wengine ambao walikuwa wanapotea.
Kijana kipindi cha nyuma ashawahi kutuhumiwa sana kutumia madawa ya kulevya na mwenyewe alikiri kabisa kutumia madawa hayo na hata aliposema ameacha lakini kuna muda bado alikuwa muonekano wake unatia mashaka.

Nahisi katika kitu ambacho alikuwa anahitaji youngdaresalama ni MANAGEMENT ambayo itasimamia muziki wake na maisha yake binafsi kitu ambacho nahisi alikuwa mwanzoni anakikosa ndo mana alikuwa anaonekana kama anapotea.

Natamani kumpa jina jipya la YOUNGAFRICAN mana nadhani ni moja ya msanii ambaye huenda tukamuona katika level za mbali kwa sasa.

Nahisi watu ambao wanasimama kama MANAGEMENT ya Young D kwa kipindi hiki ndo watu sahihi ambao walitakiwa kuwepo na kusimama naye toka mwanzo watu ambao hawasimamii muziki wake tu bali na maisha yake.

Toka kazi ya BONGO BAHATI MBAYA nahisi kila siku naona hatua za mbali sana za kijana huyu.Kujiweka mbali na tabia chafu za kuonekana ovyo kitaa, kuwa na wanawake wasiojielewa, kutojua thamani yake, kuwa na marafiki wabovu nadhani ndo kitu management ya mwanzo walishindwa kukizuia ila hii imefanikiwa kumsafisha kijana.
Nadhani kijana sasa hivi ratiba yake kubwa ni kazi tu za muziki wake zile ratiba za kipuuzi zishafutika kichwani ndio mana hata mashine hii ya #KIUTANI_UTANI Iinakuja kuwa kazi nyingine kubwa ya kumbeba tena baada ya BONGO BAHATI MBAYA.

YOUGNG D wewe ndio kijana wa kwanza kutoa mwamko kwa vijana wadogo wengi kufanya muziki ilikuwa inaleta picha mbaya kuona kijana ambaye amewa amasa vijana wadogo kufanya muziki anapotea wakati bado mdogo kwenye hii sana ya musiki.

Huu ni muda wako wa kuwaaminisha watu waliokuwa wanasema kwako haiwezekani wajue inawezekana tena sana endelea kuwa mwamko kwa vijana wadogo.

KIJANA ALIKUWA ANAHITAJI MANAGEMENT SIO YA MUZIKI TU BALI NA MAISHA YAKE.

HUU NDO MUDA SAHIHI WA KUONESHA KUWA WEWE UNA FAIDA GANI KWA TANZANIA.

Post a Comment

 
Top