Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
August 31 2017 kesi ya Mwigizaji Wema Sepetu kuhusu bangi iliendelea tena kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo mpaka mwisho Mahakama hiyo ilikataa kupokea vielelezo vya ushahidi wa msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema Mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro “Nakubaliana na hoja kwamba msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua Mahakamani“
Hiyo imekua habari njema kwa Wema Sepetu na wengine walie upande wake ambapo baada ya maamuzi hayo ya Mahakama Wema Sepetu alionekana mwenye furaha na kukumbatiana na wafuasi wake akiwemo Mama yake mzazi.
Alichokisema baada ya kutoka Mahakamani ni hiki “nimefurahi kwasababu naona kabisa kwamba haki inatendeka, nawashukuru Mawakili wangu, tunasubiria hiyo siku September 12″

Post a Comment

 
Top