Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Malkia wa filamu Bongo na Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Sepetu amefunguka hali anayokabiliana nayo ya kutopata mtoto hadi sasa.
Muigizaji huyo ambaye hivi karibuni alizindua filamu yake mpya ‘Heaven Sent’, ameiambia E-Newz ya EATV kuwa anaamini siku moja atapata mtoto kwani ni kitu ambacho amekuwa akihitaji tokea ana umri wa miaka 24.
“Kiukweli napenda nimpate mtoto hata sasa hivi kwa sababu nimekuwa nikataka mtoto tokea na miaka 24 sasa hivi na miaka 29,” amesema Wema.
“Ni ndoto lakini nasema sijakata tamaa Mwenyenzi Mungu najua ana mipango yake na ukikataa sana tamaa unamkufuru Mwenyenzi Mungu na mimi mtoto wa kislam, acha tuone itakavyokuwa,” ameongeza.
February mwaka jana Wema alidaiwa kubeba ujauzito wa mchekeshaji Idris Sultan na kuzua gumzo kubwa mitandaoni, hata hivyo baadaye uliripotiwa kuharibika.

Post a Comment

 
Top