Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga (kushoto), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA Charles Kichere(kulia) Naibu Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo wakiangalia Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akipata maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.


Sehemu ya Mzigo huuo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege ambao thamani yake ni zaidi ya Tsh. Bilioni 64.Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akizungumza wakati akipokea Ripoti ya Uchunguzi wa Madini hayo ya Almasi jijini Dar es Salaam.


Profesa Abdulkarim Mruma akiwasilisha Taarifa yake ya Uchunguzi wa Madini yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Maalum


Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wanahabari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza, kufuatilia Almasi iliyokamatwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi huku ikiwa imethaminiwa chini ya kiwango katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Naibu Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere na Kushoto kwake ni Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano na kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. John Biswalo.

Post a Comment

 
Top