Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, leo Septemba 15, 2017 ameelezea juu ya kusikitishwa kwake na tukio la kinyama la kushambuliwaji kwa kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu na watu wasiojulikana.
“Kufuatia tukio la kushambuliwa kwa Mbunge mweznetu, Tundu Lissu, naungana na Rais John Pombe Magufuli, makamu wa rais, spika, wabunge na Watanzania wote kumpa pole kwa majeraha na maumivu na majeraha makubwa aliyoyapata, tunamuombea apone haraka ili aweze kurejea kuungana na familia yake na sisi bungeni.
“Pia natoa pole kwa Meja Jenerali Mstaafu, Vincet Mritaba kwa kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Lugalo.
“Nasisitiza kwamba, serikali inawasaka na itawatia nguvuni wote wale wote waliohusika na mashambulio hayo,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Post a Comment

 
Top