Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli akipokea toka kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa ripoti mbili za Kamati Maalum za Bunge zilizofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite hapa nchini, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia katikati ni Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea ripoti mbili za Kamati Maalum za Bunge zilizofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti za kiuchunguzi za Biashara ya Madini ya Tanzanite na Almasi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti za kiuchunguzi za Biashara ya Madini ya Tanzanite na Almasi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Tanzanite hapa nchini Mheshimiwa Dotto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi hapa nchini Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mheshimiwa John Pombe Magufuli (katikati), katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa (kulia) na Spika wa Bunge Job Ndugai (koshoto), Mweyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi hapa nchini Mhe Mussa Azzan Zungu na Mweyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Tanzanite hapa nchini Mhe Dotto Biteko na Wajumbe wa Kamati zote mbili (waliosimama) mara baada ya kuzipokea ripoti hizo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Picha na Ofisi ya Bunge

Post a Comment

 
Top