Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwigizaji mkali Bongo, Wastara Juma akijiachia kimahaba na kijana mdogo (kibenteni).
DAR ES SALAAM: Makubwa! Ikiwa ni siku chache tangu amwagane na aliyekuwa mchumba’ke wa ‘kuvaliana tisheti’, Bond Suleiman Bin Sinaan, mwigizaji mkali Bongo, Wastara Juma anatengeneza tena kichwa cha habari baada ya picha zake akijiachia kimahaba na kijana mdogo (kibenteni) kunaswa na gazeti hili, twende aya kwa aya. Jumatatu ya wiki hii, mwandishi wetu akijiandaa kuondoka ofisini, mishale ya saa moja usiku, alipokea simu kutoka kwa ‘snichi’ makini kuwa, Wastara yupo maeneo ya Mwenge akiwa na bwa’mdogo huyo wakioneshana vitendo vya kimahaba huku wakipigwa picha.Njooni huyu dogodogo naona ndiyo mtu wake sasa hivi maana kila anapozunguka anakuwa naye, tena bahati nzuri huyu waliyemuomba awapige picha za kimahaba ni mshikaji wangu, amepiga kwa simu yake kisha amewarushia katika simu zao na yeye amebaki nazo.
Wakiongea jambo.
“Sasa kwa kuwa yeye hajui haya mambo ya ubuyu, mimi nimemrubuni hapa fasta kwa kumzuga natumia simu yake kisha nikazituma katika simu yangu kwa hiyo msiwe na wasiwasi kama mkiwakosa, nitawapa nilizoziiba,” kilisema chanzo hicho. Mwanahabari wetu alifika fasta katika eneo walipokuwepo na kuwakuta Wastara na ‘mtu wake’ huyo wakiwa ndani ya gari wakijiandaa kuondoka eneo hilo. Hata hivyo, Wastara alipomuona mwanahabari wetu, alishusha kioo na kuanza kumsema kwamba kama amefuata tukio ameumbuka maana wanaondoka zao.
Hata hivyo, Wastara ambaye alikuwa ameketi katika siti ya abiria ya gari hilo wakati bwa’mdogo huyo akiwa katika siti ya dereva, aligeuka mbogo baada ya kuambiwa kwamba kuna mtu amemwaga ubuyu kuwa walikuwa wakijiachia kimahaba hivyo habari hiyo itaandikwa. “Acheni mambo yenu, ina maana mimi siruhusiwi kuwa karibu na mtu yeyote au kuna mtu anayenipangia niende wapi, niwe na nani na kwa sababu zipi? “Mbona mnakosa
mambo ya maana ya kuulizana na kama mnataka tuvunjiane heshima endeleeni, yaani hadi nashangaa jamani.
“Huyu kijana ni mtu ninayefanya naye kazi, tena ni prodyuza wa muziki na muongozaji mkubwa tu wa filamu, makazi yake yako nchini China, lakini kwa sasa yuko hapa Bongo kubadilisha mfumo wa filamu zetu kwa kuongeza ubora katika video na picha, lakini pia amesomea mambo haya ya sanaa. “Kwa kuwa mimi ni mhangaikaji, nahangaika kwa ajili ya wanangu na hali hii niliyonayo, nikaona ni vyema niwe naye karibu kwa kuunganisha nguvu ili angalau tuboreshe kazi zetu.
Wakifanya yao.
“Tulipokuwa tukivurunda kwenye ubora wa kazi zetu mlisema, sasa wanapokuja wenye maarifa na uelewa mkubwa tukiwa nao karibu mnaanza kuingiza mambo yenu ya ajabuajabu, tulikuwa Mwenge kuna mahitaji aliomba nimsindikize akanunune, tukiwa kwenye gari kuna picha alikuwa ametumiwa akawa ananionesha,” alisema Wastara kwa hasira.Mwanahabari wetu alipombana zaidi na kumwambia kuna mtu amewaona wakivuka mipaka hadi ya kubusiana na picha zipo, Wastara alifunguka: “Kuhusu busu nina mipaka ya kumbusu mtu, wewe huwezi kumbusu hata dada yako kwa mfano?,”Alihoji Wastara na kumalizia: “Sikia, huyu kijana anaitwa Jukya, ana familia na mkewe, kama kuna mtu amewatuma kutuharibia kazi zetu na kututoa kwenye mstari, mmeshindwa na hamuwezi. Najiheshimu na kwa sasa naangalia kazi.
“Hivi juzi nimetoka kutoa wimbo wangu wa Mwanamke nikiwatia nguvu wanawake waliovunjika mioyo, leo tena unaniuliza habari hizo, ole wako uandike, nitaingia na tingatinga hapo ofisini kwenu, mimi ni kichaa,” alisema Wastara kisha kumuamuru bwa’mdogo huyo waondoke eneo hilo. Licha ya kukosa zile picha walizopiga kimahaba, mwanahabari wetu alifanikiwa kupata picha alizokuwa amepewa na snichi wake ambazo zimepamba ukurasa wa nyuma wa gazeti hili.

Post a Comment

 
Top