Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wakijifanya wamerukwa na akili baada ya kuiba gari.
KATIKA jiji la Mombasa, kuliibuka kioja cha aina yake siku ya Jumanne baada ya kuonekana wanaume wawili walioukuwa uchi wa mnyama. Na wote walisemekana kurukwa na akili baada ya kuiba gari la mwanamke mmoja.Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya na Tanzania, inawaonyesha vijana hao wakicheza kulizunguka gari waliloiba, mmoja wao akiwa amembeba nyoka shingoni, na kundi kubwa la watu likishuhudia kisanga hicho.Ili kurudishiwa akili zao, mwanamke mganga alidai dola 1000 za marekani sawa na shilingi 2,300,000 za Tanzania.
Gari walilodanganya kuliiba.
Hata hivyo, baadaye polisi ilibaini kisa hicho kuwa ni uongo uliotengenezwa kwa lengo la kutapeli na kufanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote wanne ambao ni: wanaume wawili waliojifanya kurukwa na akili, mwanamke aliyeibiwa gari, na mwanamke aliyejifanya mganga. Pamoja na makosa hayo, mganga huyo amekutwa na shitaka jingine la kumiliki nyara za serikali bila leseni.

Post a Comment

 
Top