Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wizara inawaasa wazazi, walezi na jamii kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watoto katika ngazi ya mitaa, vijiji na jamii ili kuwa na mifumo madhubuti katika kudhibiti ukatili unaofanywa dhidi ya watoto na kusababisha majonzi makubwa kwa wazazi, familia na jamii kwa ujumla.
Jamii inakumbushwa kuwa tatizo la utekaji wa watoto linahitaji juhudi za pamoja katika kupambana nalo ili kuzifanya jamii zetu kuwa mahala salama kwa watoto wetu kuishi. Wizara itaendelea kuimarisha Kamati za ulinzi na usalama wa Mtoto katika ngazi za kata, vijiji na mitaa ili kuboresha huduma za ulinzi wa watoto wetu. Aidha, Wizara inalipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zilizofanyika za kutaka kuwaokoa watoto hao wakiwa hai, ingawa juhudi hizo hazikufanikiwa. 
Wizara inaomba wazazi, walezi, familia, walimu na marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
07/09/2017.

Post a Comment

 
Top