Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Marehemu Ivan Don Enzi Za Uhai Wake
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Ikiwa ni miezi mitatu sasa tangu kufariki dunia kwa mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Ivan Ssemwanga ‘Ivan Don’, ambaye alikuwa mume na mzazi mwenza wa ZarinahHassan ‘Zari The Boss Lady’, akaunti yake ya Instagram imezua taharuki kutokana na picha iliyopostiwa ya watoto wake, wakati dunia nzima ikijua kwamba mmiliki wa akaunti hiyo ni marehemu.

ISHU YA KUFEKI KIFO YAIBUKA UPYA!
Baada ya picha hiyo kusambaa mitandaoni ndipo ikaibua upya lile sakata lililwahi kuvuma kipindi cha msiba wake, kwamba amefeki kifo kwa ajili ya maslahi yake binafsi, mpaka likasababisha polisi wa kimataifa nchini Uganda, Interpol kutangaza kufukua kaburi lake.
Lakini muda mfupi baada ya picha hiyo, kupitia akaunti hiyo, yakatolewa maelezo yanayomaanisha kwamba akaunti hiyo kwa sasa, inamilikiwa na mtu mwingine, japo haikufafanuliwa kama ni ndugu yake au mmoja kati ya marafiki zake kutoka kwenye Kundi la Rich Gang, alilokuwa akiliongoza.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Marehemu Ivan Don ni raia wa Uganda, alizaliwa Disemba 12, 1977, mwaka 2002 alihamia Afrika Kusini, alipata umaarufu mkubwa kupitia uwekezaji wake ambapo alifungua vyuo katika miji mitatu ya Afrika Kusini,kutokana na uwekezaji huo alikuwa akiingiza zaidi ya shilingi milioni 700 kwa mwezi.
Marehemu Ivan alipata shambulio la moyo na ndiyo tatizo hasa lililosababisha kifo chake, usiku wa kuamkia Mei25, 2017 akiwa katika Hospitali ya Steve Biko iliyopo Pretoria nchini Afrika Kusini.
Alifunga ndoa na Zari, wakafanikiwa kupata watoto wa kiume watatu, Raphael, Pinto na Quincy.

Zari Akiwa Na Watoto Wake.

Post a Comment

 
Top