Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Staa wa kimataifa wa Hispania mwenye asili ya Brazil anayeichezea Chelsea ya England Diego Costa ambaye kwa siku za hivi karibuni ameripotiwa kuwa katika mvutano na club yake ya Chelsea kiasi cha kugomea kurudi, leo September 5 2017 Costa amerudi London.
Costa amerudi London ikiwa ni siku moja imepita toka Chelsea watangaze kuwa watamfungulia mashitaka kama ataendelea kugoma kurudi na kudai fidia ya pound milioni 50, hivyo ameamua kurudi baada ya uhamisho wake wa mkopo kurudi Atletico Madrid.
Diego Costa akiwa na kocha Antonio Conte
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Diego Costa ambaye alipigwa faini na Chelsea kwa kutojumuika na wenzake wakati wa Pre Season, alianza kugomea kurudi Chelsea baada ya kudai kuwa amepokea meseji kutoka kwa kocha wa Chelsea Antonio Conte na kumueleza kuwa hayupo katika mipango yake.
Diego Costa enzi hizo akiwa Atletico Madrid
Diego Costa hivi karibuni akihojiwa na Sportsmail alieleza kuwa Chelsea wali-mtreat kama muhalifu na angerudi angekuwa akifanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha akiba, hivyo kurudi kwake London ambako ndio makao makuu ya club yake yalipo ni kutokana na kwenda kujiweka fiti ikiaminika ataondoka January.

Post a Comment

 
Top