Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Baada ya msanii wa Bongo Flava, Witness ‘Kibonge Mwepesi’ kuachia picha zenye utata/utupu katika mitandao ya kijamii mpenzi Ochu Shaggy ameshindwa kunyoosha maelezo kuhusu picha hizo kwa kudai hajawahi kuziona.
Muimbaji huyo amesema kuwa huwa hapendi kufuatilia anachoweka mpenzi wake katika mitandao na ndio sababu ya kutojua hilo ingawa wapo pamoja.
“Nimeziona kwa bahati mbaya, sipendi kuingia kwenye akaunti yake kuangalia ameposti nini, natamani ningeweza kuwaambia watu msiwe mnanitag na bahati nzuri wakati anaposti hizo picha sikuwa online karibu siku tatu na sikujua hata wakati anapiga hizo picha na anaposti,” amesema.
“Huwezi kuamini, kwanza sioni cha ajabu sana sijui kwa sababu namjua. Nikiingia Instagrama nashughulika na michogo yangu ya biashara ama stori zangu zinazohusiana na muziki,” ameongeza.
Mwaka jana Witness pamoja na Ochu Shaggy waliachia wimbo ‘Sharifa’ ukiwa ni maalum kwa ajili ya kupinga mimba za utotoni.

Post a Comment

 
Top