Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
(Picha ya jana Kabla Lissu hajashambuliwa)
Dodoma.Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameeleza alichoambiwana Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana Alhamisimchana wakati wakitoka bungeni huku
wakichekaNape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe niwatuhumiwa, hama CCM mjomba.Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini jana wakati Lissu akipelekwa Kenya alisema ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Ndege iliyomsafirisha iliondoka katikaUwanja wa Ndege wa Dodoma saa sita na robo usiku.

Post a Comment

 
Top