Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MCHEKESHAJI maarufu nchini, Emmanuel Matebe Mathias ‘MC Pilipili’ amepata ajali mbaya ya gari katikati ya Kijiji cha Nyasamba na Bubiki mkoani Shinyanga wakati akiwa njiani kurejea Dar.
Kwa mujibu wa Meneja wake, Salum Kim ambaye amezungumza na Global TV Online amesema;
“Ni kweli MC Pilipili amepata wakati dereva wake akimkwepa mtoto aliyekuwa akiendesha baiskeli.Lakini mpaka sasa tunavyoongea wamemrudisha katika Hospitali ya Bugando Mwanza na anaendelea na matibabu.
“Ameumia lakini siyo sana, zaidi alipatwa mshtuko mengine ni majeraha na michubuko aliyoipata wakati wa ajali hiyo, lakini anaendelea vizuri. Dereva wake yeye anaendelea vizuri,” alisema Salum.

Post a Comment

 
Top