Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Benny Kinyaiya.
DAR ES SALAAM: MTANGAZAJI maarufu Bongo, Benny Kinyaiya ameingia kwenye kashfa nzito baada ya video yake akiwa anapapasana kimahaba na mrembo wa Bongo Muvi, Suzan Michael ‘Prettykind’ kuvuja na kuzua mshangao.Chanzo makini kilieleza kuwa video hiyo ya Benny na mrembo huyo walijirekodi kwa ajili ya mahaba yao lakini mrembo huyo aliamua kumfanyia kitu mbaya kwa kuivujisha mitandaoni na kusababisha ugomvi mkubwa kwenye familia ya mtangazaji huyo.Yaani unaambiwa Benny na mwanamke wake hapakaliki ndani maana mke aliiona ile video kwenye mitandao ya kijamii na kucharuka hatari,” kilidai chanzo hicho.
Benny Kinyaiya.
Baada ya kupata ubuyu huo, Ijumaa lilimtafuta Benny ambaye alionyesha kusikitishwa na kitendo hicho na kusema inawezekana mrembo huyo ndiye aliyevujisha ila bado yupo kwenye kulifanyia uchunguzi suala hilo.Kiukweli hata sielewi imekuwaje, niko nafanya uchunguzi wa kina nijue ni nani aliyevujisha hiyo video, kwa sasa siwezi kusema ilikuwa ni wapi ngoja maana jambo hili limenichanganya,” alisema Benny.Kwa upande wa mrembo huyo alipotafutwa na gazeti hili alisema hajui aliyeisambaza video hiyo ila hana uhusiano na mtangazaji huyo.
Alipobanwa imekuwaje kujiachia akiwa na kanga moja na mtangazaji huyo kitandani, mrembo huyo alijiumauma kabla ya kukata simu.

STORI: GLADNESS MALLYA, DAR

Post a Comment

 
Top