Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wolper.
BAADHI ya mastaa Bongo wamekuwa na tabia ya kubadilisha wanaume baada ya muda mfupi wanapokuwa nao kwenye uhusiano wa kimapenzi kitu ambacho kinaleta picha tofauti kwenye jamii ambayo wanawaangalia wao kama kioo cha jamii na kuwafanya waonekane kama watu ambao hawana mafunzo yoyote.Kipindi hiki imekuwa kama fasheni kwa baadhi ya mastaa kuchuana live kwa mitungo ya ngono, yaani wanaanika uhusiano na mpenzi huyu jamii yote inajua kisha baada ya kipindi f’lan wanatemana na kuanzisha na mwingine.Katika makala haya, nachambua mastaa saba ambao wanachuana live kwa mitungo ya ngono;
Wastara.
WASTARA
Unaweza kusema naye ana bahati mbaya katika mlolongo mzima wa kimapenzi tangu afariki mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’. Mara nyingi anapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu anaishia kuumizwa kitu ambacho kinamfanya kutodumu na mpenzi mmoja.Ikumbukwe kuwa, baada ya Sajuki kufariki aliingia kwenye mapenzi na msanii mwenzake, Bond Suleiman ambaye naye hawakudumu muda mrefu wakaachana na hatimaye aliolewa na Mbunge wa Donge, Sadifa Juma.
Kwa mbunge huyo napo hakudumu, alikaa naye kwa muda mfupi kisha wakaachana na kumrudia Bond.Juzikati alitemana na Bond kila mmoja akimtupia maneno mazito mwenzake lakini kwa sasa ameamua kuupoza moyo wake kwa kuingia katika penzi jipya na ‘serengeti boy’ aliyefahamika kwa jina la Jukya.
Nisha.
NISHA
Salma Jabu ‘Nisha’ ni mmoja wa waigizaji wazuri wa vichekesho na maigizo lakini na yeye hakuwahi kuwa na mlolongo mzuri wa wanaume aliotoka nao kimapenzi.
Alianza kuanika uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambapo uhusiano wao haukudumu. Alikaa kimya kwa muda akaibuka na msanii mwingine, Barakah The Prince ambaye naye hakudumu muda mrefu na sasa yupo katika penzi jipya na ‘serengeti boy’ anayejulikana kwa jina moja la Minu.
Wolper.
JACQUELINE WOLPER
Ni mmoja kati ya mastaa ‘grade one’ kwenye filamu Bongo, kama ilivyo kwa Wastara na Nisha, uhusiano wake wa kimapenzi umekuwa hauna mzani uliotulia kwa kuwa mara nyingi amekuwa akibadilisha wanaume muda mfupi tu anapokuwa ameingia nao kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Nyuma kidogo staa huyo ambaye ana msururu mkubwa wa wanaume waliompitia alikuwa penzini na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize lakini hawakudumu muda mrefu waliachana na kugeukia penzi jipya la kijana anayefahamika kwa jina moja la Brown.
Uwoya.
UWOYA
Anaingia kwenye orodha ya mastaa wenye mtungo wa kimapenzi baada ya kusikika kwa skendo zake mbalimbali za kimapenzi tangu alipoachana na mumewe, Hamad Ndikumana.
Baada ya kutemana na mumewe, alisikika kutoka kimapenzi na mwanamuziki Linex kisha Msami Baby, Quick Racka na juzikati alihusishwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki Dogo Janja.
Kajala.
KAJALA
Kama ilivyo kwa mastaa wengine hapo juu, Kajala naye ni miongoni mwa mastaa wanaoongoza listi ya kuchuana kwa kuwa na msururu mrefu wa wanaume.
Alishawahi kuwa na uhusiano na Petit Man, CK na baadaye msanii wa Bongo Fleva, Quick Racka.
Shilole.
SHILOLE
Ni miongoni mwa mastaa waliopo kwenye listi ya kuwa na uhusiano na wanaume tofautitofauti ndani ya kipindi kifupiIkumbukwe kuwa alianza uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Barnaba kisha Nedy Music ambaye hakudumu naye na kuingia katika penzi na Nuh Mziwanda.
Hata hivyo hakudumu na Nuh, akaingia katika penzi jipya na msanii mwingine, Hamadai kisha akaenda Mr Kesho kabla ya hivi karibuni kuhamia kwa mwanaume anayefahamika kwa jina la Uchebe.
Wema.
WEMA
Naye anaibeba listi ya mastaa ambao hawadumu katika mapenzi, mrembo huyu alianza kuhusishwa kuwa katika uhusiano na wasanii Mr. Blue na TID kabla ya kuingia kwa marehemu Kanumba.
Hakudumu na Kanumba akaingia kwa mjasiriamali, Jumbe Yusuf ambaye alitangaza hadi ndoa iliyokuja kuyeyuka ghafla. Baada ya Jumbe, Wema alizama kwa msanii wa Dansi, Chaz Baba ambaye naye hakudumu na kuzama kwa msanii wa Bongo Fleva.
Haikuishia hapo, aliingia kwa mshiriki wa Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Luis Mnana ambaye ni raia wa Namibia ambapo hawakudumu na kuingia kwa Idris.
MAKALA: Imelda Mtema

Post a Comment

 
Top