Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

"Usiku wa kuamkia leo
ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa.Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu.Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama Nchi, Kama Taifa.Kilichotokea na kumpata ndugu yetu Lissu jana, ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana kabisa na utamaduni wetu wa ustahimilivu na undugu ambao nchi yetu imekuwa ikisimamia.Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia.Watanzania tunaolitakia mema taifa hili tuna kila sababu ya kulaani na kukataa kabisa utamaduni huu wa kimafia kuzoeleka katika taifa letu.

Tusimame kulaani kwani #HuuSiUtanzania"

Post a Comment

 
Top