Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Wakongwe wa Manchester United wakiongozwa na Ruud van Nistelrooy wametoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya wale wa FC Barcelona waliokuwa wakiongozwa na Patrick Kluivert.Hii ilikuwa ni mechi ya pili baada ya ile ya kwanza kwenye Uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona ambako wenyeji walipoteza kwa maba0 2-4.Katika mechi ya leo kwenye Uwanja wa Old Trafford ambayo Saleh Ally “Jembe” alikuwa kati ya waalikwa, wenyeji ndiyo walianza kufunga mabao mawili hadi mapumziko.Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson alikuwa kati ya walioshuhudia mechi hiyo hadi mwisho.
 Bao la kwanza liliwekwa kimiani na Van Nistelrooy kwa mkwaji wa penalti baada ya Karel Poborsky kuangushwa na Danny Webber akafunga la pili.

Lakini kipindi cha pili, FC Barcelona wakasawazisha kupitia Luis Garcia ambaye pia aliwahi kuichezea Liverpool na Gaizka Mandieta ambaye alikuwa kiungo muhimu kwa upande wa Barcelona leo.


Barcelona: (4-3-3): Angoy; Belletti, Edmilson, Dehú, Abidal; Davids, Sergi, Mendieta; Simao Kluivert, Goiko
Goals: Luis Garcia, Mendieta
Manchester United (3-4-2-1): van der Sar; Brown, Dublin, Johnsen; Park, Poborsky, Yorke, Silvestre; Blomqvist, Saha; van Nistelrooy
Goals: Van Nistelrooy (Pen), Webber


Post a Comment

 
Top