Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jumba la Lugumi.
KAMPUNI ya Udalali ya Yono leo Septemba 9, 2017 itapiga mnada maghorofa yanayomilikiwa na kampuni ya Lugumi. Maghorofa hayo mawili yapo maeneo tofauti moja likiwa Mtaa wa Mazengo Upanga na lingine likiwa Mbweni jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Yono, Scolastica Kevela amesema leo Ijumaa kuwa wametumia njia mbalimbali ili kufanikisha mnada huo kufanyika hasa kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Lugumi.
Amesema hawezi kutaja gharama halisi ya mali hizo na deni ambalo kampuni hiyo inadaiwa na Mamlaka ya Mapato(TRA) hivyo hao ndio wanaoweza kutoa majibu hayo.
“Kazi yetu sisi ni kupiga mnada tu, gharama ya deni na thamani ya mali hizo TRA ndio wanatakiwa kutolea majibu,” alisema Kevela.
Alisema fedha watakazozipata zitakwenda kusaidia nchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo

Post a Comment

 
Top