Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa muziki Bongo, Linah Sanga ameeleza baadhi ya mambo yanayomfurahisha na kumtatiza kutoka kwa mwanae.
Muimbaji huyo ambaye alijifungua July mwaka huu ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa mwanae ni mpole kupitiliza ila anachelewa kulala.
“Ni mpole sijui nisemaje, akishanyonya tu anatulia anaweza kukaa kimya mpaka tukashangaa, watu wanasema atabadilika lakini kadiri tunavyozidi kwenda ndio anazidi kuwa mpole,” amesema Linah.
“Usumbufu wake yeye ni kukaa macho, sasa mama huwezi ukalala mwanao yupo macho, kwa hiyo unabidi usubiria mpaka yeye asinzie ndio na wewe ulale,’ ameongeza.
Pia Linah amesema hadi sasa mwanae ni balazi wa kampuni fulani ya pampasi, duka la nguo na duka la mafuta ya nazi.

Post a Comment

 
Top