Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamuziki Linah Sanga akiwa na familia yake.
ESTERLINA Sanga ukipenda waweza kumuita Linah au Ndege Mnana, ni mmoja wa mastaa wa Muziki wa Bongo Fleva aliyepotea kwa muda kutokana na pilika za uzazi. Linah anayebamba na nyimbo zake nyingi zikiwemo No Stress, Kosa Sina, Raha Jipe Mwenyewe na Malkia wa Nguvu kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja aliyempa jina la Tracy Paris ambaye amezaa na mchumba anayefahamika kwa jina moja la Shaban.
Ijumaa limemfungia kazi na kufanya naye mahojiano moja kwa moja akiwa kwenye studio yake pande za Tegeta jijini Dar na katika makala haya amefunguka mengi likiwemo la kutaka kuolewa na mchumba wake huyo ambaye wapo tofauti kiimani.
Ijumaa: Wanamuziki wengi wamekuwa wakijishauri sana katika suala zima la kubeba ujauzito kutokana na kazi zao, wewe halikukuumiza kichwa hili?
Linah: Kwa sababu niliamua kwa moyo mmoja kabisa wala hilo sikujiuliza hata mara moja kwa kuwa nilitamani mtoto.Ijumaa: Wakati unaelekea chumba cha kujifungua, muda mfupi kabla ya kuingia uliposti picha ukiwa kwenye uchungu, haikukuletea matatizo hasa kutokana na mila zetu?
Akiwa katika pozi
Linah: Kwanza ile picha sijaiposti nafikiri kulikuwa na mtu pale hospitali na pia haikuwa siku ambayo najifungua ilikuwa ni siku ambayo nilienda kuonana na daktari, sikuwa najisikia vizuri.
Ijumaa: Baba watoto wako yeye sio staa?
Linah: Hapana wala hayuko huko kabisa.
Ijumaa: Sasa mnawezaje kuendana maana mastaa kuna mambo mengi?
Linah: Unajua huyu mchumba wangu alinipenda tangu 2009, ndio kwanza naanza kutoka lakini hakupata muda wa kunifikia hivyo anajua kazi yangu na ndio maana niko nae amekubali kila kitu changu.
Ijumaa: Vipi kuhusu ndoa wewe na mchumba wako kuna matarajio hayo?
Linah: Ndiyo ni hivi karibuni.
Wakiwa na mume wake Shaban
Ijumaa: Lakini mpenzi wako ni Muislam na ninajua wazi kuwa wewe umetoka kwenye familia ya Kikristo inakuaje hili?
Linah: Ni kweli ni Muislam lakini sioni shida kuolewa naye.
Ijumaa: Kipindi cha ujauzito uliweka picha za kuonesha tumbo wazi, hiyo haikuleta shida kwa wakwe zako?
Linah: Namshukuru sana Mungu, nimepata wakwe waelewa sana kikubwa wao wanataka heshima wala hilo la picha hawalitazami.
Ijumaa: Wewe na msanii Amini mlikuwa wapenzi mnaopendana sana, vipi mkikutana sasa hivi?
Linah: Mimi na Amini tunaheshimiana sana kwa kuwa tayari ana mke wake na mimi nina mtu wangu.

Ijumaa: Asante kwa ushirikiano wako

Post a Comment

 
Top