Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ligi ya Mabingwa Ulaya imerejea, sasa ni msimu wa 2017/18, vigogo wote watakuwa uwanjani leo na kesho, beki wa PSG, Thiago Silva ameenda mbele zaidi kwa kusema presha ni kubwa kikosini kwao kutokana na usajili uliofanyika.Silva anasema ujio wa Neymar na Kylian Mbappe utawafanya wawe na presha kubwa kwa kuwa watu wengi watahitaji mambo makubwa kutoka kwenye timu yao ambao inatarajiwa kukipiga dhidi ya Celtic katika michuano hiyo.
PSG ipo nchini Scotland kwa ajili ya mchezo huo, ambapo wababe hao wa Ufaransa, Paris Saint-Germain watakuwa na nia moja tu ya kupata ushindi kwa kuwa mastaa waliosajiliwa ni w agharama kubwa.
“Tumeshasahau yaliyopita katika msimu uliopita, tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huu na muhimu ni kupata paointi tatu,” alisema beki huyo wa kati.






Wachezaji wa timu ya Manchester United wakifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani na wageni Basel.




Ratiba ya michezo ya leo Jumanne ambayo yote itaanza saa 3:45 Usiku ni hii hapa

Celtic v PSG 
Benfica v CSKA 
Manchester United v Basel
Olympiakos Piraeus v Sporting CP
Bayern München v Anderlecht
Chelsea v Qarabağ 
Roma v Atlético Madrid 
Barcelona v Juventus

Ratiba ya kesho Jumatano
Maribor v Spartak 
Tottenham v Borussia Dortmund
RB Leipzig v Monaco
Feyenoord v Manchester City
Shakhtar v Napoli 
Real Madrid v APOEL 
Liverpool v Sevilla Anfield
Porto v Beşiktaş

Post a Comment

 
Top