Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Malkia wa Bongo Flava Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, amebainisha sababu zilizomfanya ku-rap katika ngoma yake mpya aliyoachia mapema wiki hii.amesema kuwa kama msanii huwezi kufanya vitu vilevile kila ili watu wakuone mpya lazima ubadilike.
“Sababu ya kufanya rap ni kwa sababu huwezi kufanya vitu vilevile kila siku, ili watu wakuone ni mpya na wapende kitu kipya lazima ufanye kitu ambacho ni tofauti na ulichokuwa unakifanya,” amesema Jide.Pia akaongeza kuwa verse ya kwanza ya ngoma hiyo imeandikwa na rapper One The Incredible.
Video ya ‘I Miss You’ inatarajiwa kutoka hivi karibuni na huu ni ujio wake mpya wa mrembo huyi ikiwa ni baada ya kuachia albamu yake ya saba, iitwayo ‘Woman’ mwezi wa nne mwaka huu.

Post a Comment

 
Top