Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jumapili ya September 17 2017 nahodha wa zamani wa Man United anayeichezea Everton Wayne Rooneyatarudi kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Old Trafford baada ya kuihama club hiyo wakati wa dirisha la usajili la majira ya joto.Rooney anarudi Old Trafford ambapo ndio uwanja wa nyumbani wa Man United na Rooney ambaye alidumu na club hiyo kwa miaka 13 anarudi katika uwanja huo safari hii akiingia vyumba vya kubadilishia nguo vya timu za ugenini tofauti na alivyozoea.
Stori ni kuwa Rooney atapokelewaje na mashabiki wa Man United atakapoingia uwanjani akiwa upande wa timu pinzani, kocha wa Man United Jose Mourinho anaamini mashabiki wa Man United watampokea kwa heshima anayostahili Wayne Rooney ambaye ni ‘Legend’ wa club hiyo na mfungaji bora wa muda wote wa club hiyo.
“Nafikiri Rooney atapata mapokezi anayostahili katika mchezo wa Jumapili, Rooney ni legend wa kweli kwa magoli aliyofunga na mataji ni wazi kuwa yeye ni moja kati ya wachezaji muhimu katika historia ya ManUnited, nafikiri mashabiki watampa heshima anayostahili kabla, wakati na baada ya mechi”>>> Jose Mourinho
Paul Pogba ataukosa mchezo dhidi ya Everton kwa kuwa majeruhi

Post a Comment

 
Top