Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Siku zimeanza kuhesabika kuelekea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi June 14 2018, michuano ya Kombe la dunia huwa inafanyika kila baada ya miaka minne na mara ya mwisho kufanyika ilifanyika mwaka 2014 nchini Brazil.
Bei ya tiketi za kwenda kuangalia michuano hiyo zimetolewa leo lakini kwa mashabiki watakaohitaji watalazimika kuomba kupitia mtandao wa FIFA na tiketi zitauzwa kwa awamu mbili, kwa mechi za makundi kuanzia round ya pili itakuwa pound 79 (Tsh 237,208) hadi pound 829 (Tsh 2,489,184 ) kwa ajili ya mchezo wa fainali utakaochezwa mjini Moscow July 15 2018.
Sera za uuzwaji wa tiketi kwa mkazi wa Urusi wao wataanza kupata tiketi kuanzia pound 17 (Tsh 51,047) tofauti na raia wa kigeni watakaotaka kuhudhuria michuano hiyo, bei ya juu ya tiketi kwa ajili ya mchezo wa fainali itakuwa pound 829 (Tsh 2,489,184) ambapo imeongezeka kwa pound 151 (Tsh 453,423) ukilinganisha na bei ya tiketi za Kombe la dunia za 2014 nchini Brazil.
Watu wote watakaohitaji tiketi kwa awamu ya kwanza watapaswa kuomba kabla ya October 12 2017 na majibu ya maombi yao watapata November 16 2017, baada ya maombi itachezeshwa droo ili kupata watu watakaopata nafasi za kushuhudia michuano hiyo kwa sababu sio kila aliyeomba atapata.


Vi

Post a Comment

 
Top