Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kocha wa Chelsea Antonio Conte amefunguka na kueleza mipango yake kuelekea game ijayo ya Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal katika uwanja wao wa Stamford Bridge, Conte bado hataki kuamini kuwa ushindi wake mfululizo utamuwezesha kupata ushindi dhidi ya Arsenal.Chelsea wataingia kucheza dhidi ya Arsenal Jumapili ya September 17 2017, wakiwa wamefanikiwa kuvuna point 9 kwa kupata ushindi katika mechi zao tatu kati ya nne walizocheza za EPL, wakati Arsenal watakuwa wanaingia kucheza mchezo huo wakiwa wana point sita baada ya kushinda game mbili na kupoteza game mbili.
Katika game hiyo Chelsea watakuwa wanaingia kutafuta ushindi wa nne mfululizo wa EPL lakini wanatafuta kulinda rekodi yao ya kutopoteza nyumbani dhidi ya Arsenal toka 2011 licha ya Conte bado anakumbuka kipigo cha 2-1 cha Ngao ya hisani, hivyo hataki kuamini kuwa matatizo ya Arsenal kwa sasa yatamuwezesha kuifunga kirahisi.
“Sijali kuhusiana na matatizo ya Arsenal nafikiria kuhusu Chelsea, wanaweza wakatatua matatizo yao tunaweza kutatua matatizo yetu, sijui kwa nini hawapo katika mbio za kuwania Ubingwa wakati wamepoteza mchezaji mmoja pekee (Chamberlain)”>>>Antonio Conte

Post a Comment

 
Top