Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameamua kumuacha Philippe Coutinho katika list ya wachezaji atakaowatumia katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester City unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi ya September 9 2017 katika uwanja wa Etihad.
Jurgen Klopp ametangaza kufikia maamuzi hayo akitaja kuwa ameamua kuwa atapanga kikosi kipya na nafasi ya Coutinho anatajwa kuwa atachukua Oxlade-Chamberlain aliyejiunga na Liverpool kwa pound milioni 35 akitokea Arsenal.
Hata hivyo Jurgen Klopp ambaye amefanya maamuzi hayo anaripotiwa kufanya hivyo akiwa amekubaliana na Coutinho “Nimeamua kumuacha katika kikosi kitakachocheza dhidi ya Man City kwa ajili ya kumpa siku tano sita za mazoezi mazuri na kujiweka fiti zaidi”

Post a Comment

 
Top